Unajihisi una dalili za COVID-19?
Huu ukurasa unatoa taarifa juu ya ugonjwa wa COVID-19, dalili na namna ya kujikinga
Taarifa zote za idadi ya wagonjwa, vifo n.k zinatoka moja kwa moja kutoka Chuo Kikuu cha John Hopkins kilichopo Marekani.
ChanzoTaarifa
Hii ni taarifa ya COVID-19 ya dunia yote
Walioathirika
haijarekodiwa
Vifo
haijarekodiwa
Taarifa za tanzania juu ya corona virus
Walioathirika
haijarekodiwa
Vifo
haijarekodiwa
Dalili kuu za COVID-19 (Coronavirus)
Dalili za COVID-19 zinatofautiana kutoka kutoonesha dalili yoyote hadi kuonesha kuwa katika hali mbaya, na zinaanza kuonekana kuanzia siku 2 toka mgonjwa aambukizwe had siku 14
Kikohozi kikavu na mafua
Upumuaji wa shida
Unajihisi una dalili za COVID-19?
Uzuiaji
Kwa sasa hamna dawa wala tiba iliyothibitishwa ya COVID-19, dawa kwa ajili ya kinga bado zinafanyiwa majaribio.
Njia nzuri za kujikinga na COVID-19 ni kujiepusha na mazingira yenye hawa virusi
Fanya
- Baki nyumbani kama hakuna ulazima wa kutoka na kama u mgonjwa
- Jizuie kushika sehemu mbalimbali za uso hasa macho, pua na mdomo
- Safisha na ua vijidudu kwa kutumia dawa maalum maeneo ambayo unayagusa mara kwa mara
- Unapokohoa au kupiga chafya jizibe kwa tissue au kitambaa
- Jizuie kukaribiana na wagonjwa na vaa barakoa(mask) unapowahudumia wagonjwa wa COVID-19
- Safisha mikono yako kwa maji yanayotiririka na sabuni walau kwa dakika 20 mara kwa mara
Usifanye
- Kushikana mikono na watu, kukumbatiana, mabusu
- Kushika macho, mdomo na pua kama mikono yako sio misafi
- kwenda kwenye mikusanyiko au kwenda maeneo yenye idadi kubwa sana ya watu bali, Jizuie kadiri unavyoweza kwenda maeneo hayo